- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKILI MBARONI KWA KUTUMIA LIFTI YA RAIS KENYATTA
KENYA. WAKILI Kincy Nangami Wafula, 29, ameshtakiwa katika mahakama ya Kenya kwa kuwatusi maafisa wawili wa polisi waliomzuia kutumia njia(lift) ambayo hutumiwa na Rais Uhuru Kenyatta ndani ya jumba la KICC, mjini Nairobi.
Wakili huy alikanusha mashtaka mawili ya kutusi afisa msimamizi wa kituo cha polisi cha KICC na Sajini Susan Misoi. Bi Wafula anadaiwa kutenda uhalifu huo alipokutwa akitafuta mahala pa kujisaidia katika jumba la KICC.
Wakili huyo alikanusha shtaka la kuwatukana OCS, Catherine Otieno na Sajini Susan Misoi. Bi Wafula alikumbana na maafisa hao wa polisi alipokuwa akitafuta mahali pa kujisaidia.
Alielekezwa na mfagiaji eneo alilokutwa na maafisa hao wa polisi.
Wakati wa mahojiano alichokuwa akifanya eneo hilo lisilokubaliwa watu kutembelea, mshtakiwa aliwaeleza hakujua kwa vile yeye ni mgeni. Ni wakati huo hasira ilimpanda ndipo akawatukana polisi matusi tusiyoweza kuyachapisha.
Alikabiliwa na shtaka la kutumia lugha chafu kwa polisi na kukataa kutiwa nguvuni. Aliachiliwa kwa dhamana ya Ksh20,000 sawa na Tsh. 420,000