Home | Terms & Conditions | Help

September 20, 2024, 7:22 am

NEWS: WAFANYAKAZI WA BANDARI YA BEIRUT WAKAMATWA KUFUATIA MLIPUKO

Kufuatia mlipuko mkubwa kuwahi kushuhudia nchini Lebanon uliogharimu maisha ya watu zaidi ya 137 na 5,000 kujeruhiwa Watu kadhaa wamekamatwa wakiwemo wafanyakazi 16 wa Bandari ya Beirut.

Hundreds of Thousands Displaced By Beirut Explosion

Watu hao wote ni wafanyakazi wa bandari ya mji mkuu wa Lebanon. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Wachunguzi wanatathmini iwapo utunzaji wa kemikali aina ya ammonium nitrate, inayoaminika kusababisha milipuko hiyo mikubwa, ilifanyika kwa makusudi.

Maafisa 16 kutoka bandari ya Beirut na viongozi wa forodha wametiwa nguvuni, bila kujua tarehe halisi ya kukamatwa kwao, ameripoti mwandishi wetu RFI Bw. Pierre Olivier.

The Beirut explosion was six years in the making and hit a country on its knees

Hatua ya kukamatwa kwa watu hao ni ishara kubwa kwa raia wa Lebanon ambao wanasubiri haki itendekea na wahusika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Rais wa Ufaransa ambaye yuko ziarani nchini Lebanon ametaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kubaini ukweli kuhusu mlipuko huyo, huku akitoa wito kwa viongozi wa Lebanon 'kufanya mabadiliko makubwa' ya kisiasa.