- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WADAU WA KILIMO WAWATAKA VIONGOZI KUTEKELEZA AZIMIO LA MALABO.
DODOMA: Wadau wa Sekta ya Kilimo duniani wamewataka Viongozi wa Serikali kufuatilia shughuli mbalimbali wanazozitoa ikiwemo mafunzo , mikopo inayotolewa kwaajili ya Wakulima ili kutekeleza azimio la Malabo la wakulima katika kilimo chenye tija na manufaa kwa Taifa.
Haya yameelezwa Wakati wa Kongamano la Malabo Policy Learning Event (MAPLE) lilifanyika Jijini Dodoma lililowakutanisha wakulima Wadogo kutoka Wilaya ya Chamwino, ActionAid na Wadau wa kilimo bara la Afrika kwa njia ya Mtandao ( Video Conference)
Wadau hao walisema bado kuna changamoto katika utekelezaji wa tamko la Malabo kwa kuwa baadhi ya Viongozi kutokuwa wafuatiliaji wa shughuli zinazotolewa kwa ajili ya wakulima pamoja na mapitio ya Sekta ambayo hayajafanyika kwa kipindi cha miaka minne.
Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mkurugenzi wa Kilimo na Maendeleo Vijijini, Dk Godfrey Bahiigwa, amesema licha ya miaka sita ya utekelezaji wa Azimio la Malabo, kuna nchi chache tu ambazo zimehimiliki tangu kupitishwa.
Kwa Upande wake Mkuu wa Kilimo na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la AU, Mamadou Diakhite, amesema nchi nyingi za Afrika bado zinapambana na marekebisho ya sera huku ulimwengu ukiendelea kupambana na janga la Covid-19.
Hata hivyo, alizitaka nchi zote wanachama wa AU kuzingatia tamko la Malabo kama ajenda ya kimataifa ikiwa kumaliza umaskini ni jambo la kutatanisha.
Akizungumza kwa niaba ya sekta binafsi, Nana Honey amesema ilikuwa injini kuu katika shughuli za Kilimo na uwekezaji kuwepo wanasayansi zaidi ambao wanaweza kufanya tafiti zenye manufaa.
"Afrika ina idadi ya watu muhimu na hivyo tunahitaji ushiriki wa ndani katika sekta hii na ili hili liweze kufikiwa tunahitaji mbinu iliyoratibiwa kati ya sekta binafsi, serikali ya Afrika, Mashirika ya kiraia na wadau wengine," amesema.
Ameendelea kwa kusema ipo haja ya kuwa na rasilimali fedha za kutosha, uwekezaji katika sekta binafsi yenye uthabiti pamoja na mifumo mizuri ya kutambua mifumo ya lishe bora.
Tamko hilo lilipitishwa mwaka 2014 lakini utekelezaji wake rasmi ulianza mwaka 2015, Azimio la Malabo lililotiwa saini na Serikali za Afrika mwaka 2014 liliwakilisha kujitolea tena kwa kanuni na malengo ya Mpango Kamili wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP) iliyopitishwa mapema mwaka 2003 chini ya Azimio la Maputo.
Mwaka 2003, viongozi wa nchi za AU walikubaliana katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, kutenga kima cha chini cha asilimia 10 ya bajeti yao yote ya kitaifa kwa sekta ya kilimo ili kuhakikisha usalama wa chakula na kukabiliana na umaskini wa vijijini ifikapo mwaka 2015, Wakati wa Mkutano wa Maputo, huko nyuma. , Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Mpango uliobatizwa jina la CAADP ulibuniwa na ulilenga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inakua kwa kiasi kikubwa.
CAADP ni mfumo wa sera ya Afrika kwa ajili ya mabadiliko ya kilimo, uzalishaji mali, usalama wa chakula na lishe, ukuaji wa uchumi na ustawi kwa wote. Katika Mkutano wa AU wa Maputo, viongozi walitoa tamko la kwanza kuhusu CAADP kama sehemu muhimu ya Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (NEPAD).
Baadaye mwaka 2014, tamko la Malabo lilikwenda mbali zaidi kwa kubainisha malengo na shabaha mahususi zinazopaswa kufikiwa ndani ya kipindi cha miaka kumi. Malengo hayo ni pamoja na kumaliza njaa, kuongezeka mara tatu kwa biashara ya bidhaa na huduma za kilimo baina ya nchi za Afrika, kuimarisha ustahimilivu wa maisha na mifumo ya uzalishaji, na kuhakikisha kuwa kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini.