Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:58 pm

NEWS: WACHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO WABURUZWA MAHAKAMANI

WACHUNGAJI wa kanisa la Mlima wa Moto tawi la Buza, jijini Dar es Salaam, Patience Sunga (53) na mke wake Michou Sunga (50) wamefikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuishi nchini bila kibali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Shija Sitta mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate imedai washtakiwa walitenda kosa hilo Mei 3, 2019 huko Ilala jijini Dar es Salaam.