- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WAWILI WA CHADEMA WATIMKIA NCCR-MAGEUZI
Dodoma. Wabunge wawili, wa viti maalumu kutoka chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Suzana Maselle (Mwanza) na Joyce Sokombi (Mara),wametangaza kujiondoa kwenye chama hicho na kutimkia chama cha NCCR-Mageuzi
“Tumeamua kuondoka Chadema, mara baada ya kumaliza kipindi chetu cha ubunge, Juni mwaka huu,” ameeleza Masele,
Akiongea na Waandishi wa Habari juu ya uwamuzi wao huo leo Ijumaa Mei 22, 2020 mjini Dodoma Suzana Maselle, amesema uamuzi wao wa kuondoka Chadema, umetokana na chama hicho, kutawaliwa na ubinafsi, matumizi mabaya ya rasimali za chama na ubabe wa kiongozi mkuu wa chama hicho.
Amesema, Chadema kimekuwa kwa kasi kubwa kutokana na kuungwa na wananchi wengi kutokana na kazi nzuri iliyokuwa inafanywa bungeni na wabunge wake katika vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Amesema, hata wao walivutika kuingia bungeni ili waweze kuwa sehemu ya hao askari waliomstari wa mbele kwenye mapambano hayo. “Tulipofika bungeni tulikuta hali ni tofauti sana.
Uongozi wetu yaani KUB haukutoa fursa hiyo kwetu; badala yake, alikuwa na wateule wake wachache ambao hao ndio waliaminika zaidi na ndio waliopewa kila fursa ya kuiwakilisha kambi,” ameeleza. Kutokana na hali hiyo, Maselle amesema, “sisi tulijikuta tukiwa wasindikizaji na wasikilizaji zaidi.
Tulivumilia, Tukijua kuwa ni muhimu kuendeleza umoja wetu na pili kujifunza na kila tulipopata fursa tulionyesha uwezo wetu na kubainisha malalamiko yetu. Amesema, “maoni ya kutokuridhishwa na hali kama hiyo, yalitufanywa tutengwe na kupuuzwa zaidi.
Pamoja na yote hayo michango iliyotolewa na hao wateule mingi ni vijembe ambavyo vilituondoa kwa kiwango kikubwa kwenye agenda yetu.” Anasema, “hali hii imekuwa mbaya zaidi baada ya Esther Bulaya, kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi yetu na kujipa mamlaka yaliyopitiliza. “Kabla ya hapo, palikuwepo na kafursa kakuulizwa na kujipendekeza.
Wakati huu, ni amri tu. Kwa kifupi, maamuzi mengi ni ya kibabe na yenye kudharau watu wengine, na kwa bahati mbaya kiongozi mkuu wa chama haonyeshi kuchukua hatua kurekebisha hali hii,” ameeleza Maselle.