- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VURUGU ZA MAWAKILI ZAIBUKA KESI YA SABAYA
Katika hali ambayo haikutarajiwa kumetokea Mabishano ya Kisheria baina ya Mawakili wa Serikali na wale wanaomtetea Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili katika kesi namba 105 ya Mwaka huu.
Mabishano hayo ambayo yametokea hii leo Jumatatu Agosti 17, 2021 yametokana na ombi la Jamhuri kwamba mahakama ifanye marekebisho ya jina la mshatikawa namba moja, Lengai Ole Sabaya katika hati ya mashtaka ya July 16 kwa misingi kwamba jina lilikosewa kwa kuandikwa Lengai Ole Sayaba.
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula ameeleza Mahakama kuwa kulitokea makosa ya uandishi na kwamba hati hiyo isomeke Lengai Ole Sabaya na si Sayaba. Wakili Chavula aliomba chini ya kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria namba 234 Sura ya 20 ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2019.
Wakili upande wa Utetezi, Wakili Mosses Mahuna amesema mshitakiwa huyo alikutwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi na mshitakiwa kuanza kujitetea. Wakili Muhina amedai, upande wa utetezi hawapingi mshitakiwa namba moja, Lengai Ole Sabaya bali wanapinga mshitakiwa aliyeletwa katika hati ya mashtaka ambaye ni Lengai Ole Sayaba.
Upande wa utetezi umeendelea kudai kwamba Jamhuri ilileta mashahidi 11 na mawakili wasomi wanne wa serikali kuthibitisha hati ya mashtaka yenye jina la mshtakiwa Lengai Ole Sayaba.
Sabaya na wenzake wawili wanatuhumiwa kutenda makosa matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Sabaya na wenzake, wanatuhumiwa kutenda makosa hayo katika duka la Mohamed Saad huko eneo la Bondeni jijini Arusha, Februari 9 mwaka huu.