Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:41 pm

NEWS: VIONGOZI WA MAPINDUZI MALI WAJIWEKEA SHERIA YA KUTOSHTAKIWA

Mali. Viongozi wa mapinduzi nchini Mali wamejiwekea kinga ya kutoshtakiwa kwa namna yoyote ile na vyombo vya sheria nchini humo kuhusiana na vitendo vyao vya kuipindua serikali iliyopita madarakani, hii ni kabla ya kuundwa serikali mpya ya mpito nchini humo.

Sheria hizo zinahuhusu mapinduzi ya Agosti 2020 dhidi ya rais wa wakati huo Ibrahim Boubacar Keïta na mapinduzi ya Mei 2021 dhidi ya rais wa mpito Bah N’Daw. Viongozi wa mapinduzi, ikiwa ni pamoja na Assimi Goïta, ambaye ni rais wa mpito wa Mali, hawawezi kushtakiwa na mahakama yoyote nchinihumo kwa hatua zao dhidi ya mamlaka zilizotangulia katika vipindi hivi viwili.

Sheria ya kwanza ya msamaha inachukuwa kipindi cha kuanzia Agosti 18 hadi Septemba 24, 2020, ikimaanisha kipindi ambapo Assimi Goïta aliendesha mapinduzi ya kijeshi hadi alipotawazwa Bah N'Daw kama rais wa mpito. Sheria ya pili inahusu kipindi cha Mei 24, 2021, siku ya jeshi lilipomkamata Bah N’Daw na Waziri Mkuu wake Moctar Ouane, hadi kuachiliwa kwao mnamo Agosti.

Hakuna mashtaka

Chini ya sheria hizi, katika vipindi hivi viwili, wahusika wa vitendo vya "kutotii, njama za kijeshi, utoro" hawawezi kushtakiwa katika mahakama yoyote nchini Mali. Walakini, katika Ibara ya 121 ya Katiba ya Mali, imeweka wazi kuwa mapinduzi yoyote ni jinai isiyoweza kuhesabiwa dhidi ya raia wa Mali.

Kizuizi hiki kimeondolewa na Souleymane Dé, mwenyekiti wa kamati ya sheria ya Baraza la Kitaifa la Mpito, ambalo kwa sasa linatumika kama chombo cha kutunga sheria: "Kilicho kipya na kile ambacho kila mtu atahitaji kuelewa ni kwamba haikuwa mapinduzi ya kijeshi. Hakukuwa na mapinduzi, kwa sababu Katiba haikusimamishwa na rais alijiuzulu kwa hiari. Hakukuwa na kujiuzulu chini ya shinikizo, wala kulazimishwa, hapakuwa kitu kama hicho. Kweli, nchini Guinea kuna mapinduzi. Lakini nchini Mali, hakukuwa na mapinduzi. "

Souleymane Dé kwa hivyo badala yake anaibua "kukamilika kwa mchakato unaoendelea", kwa kurejelea maandamano ya kiraia ambayo mnamo 2020 yalitaka Ibrahim Boubacar Keïta ajiuzulu na "marekebisho ya mpito" kwa mapinduzi ya jeshi ya mwezi Mei mwaka huu