Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:09 pm

NEWS: VILABU 12 VIKUBWA ULAYA VYAUNDA LIGI YAO

Timu 12 kutoka barani Ulaya zimeanzisha michuano ya Europeansuperleague, lakini shirikisho la soka la UEFA limepinga vikali michuano hiyo, vilabu hivyo ni AC Milan, Inter, Juventus,Atletico, Barca, Real Madrid,Arsenal, Liverpool, ManCity, ManUtd, Chelsea na Tottenham.

Michuano hiyo itakuwa ikichezwa mwezi May na Agosti.

Chama cha vilabu vya soka barani Ulaya, ECA, amabcho kinawakilisha vilabu 246 Ulaya yote, kimeandika barua kwa Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA, kupinga mpango wa vilabu hivyo kuanzisha ligi yao ya Ligi Kuu ya Ulaya.

Rais wa Chama hicho ni Andrea Agnelli, ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Juventus ya Italia ambayo ni moja ya vilabu vilivyosaini kuanzishwa kwa ligi hii.

Mbaya zaidi, Agnelli ni rafiki wa karibu wa Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin, ambaye anaupinga sana mpango huu.

Ina maana Agnelli amemsaliti rafiki yake, Rais wa UEFA, lakini pia ni kama chama anachokiongoza pia amekisaliti.

LIGI YENYEWE

Ligi hii ni wazo la tangu miaka ya 1980 lakini kwa sasa liliibuliwa upya mwaka 2009 na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez pamoja na matajiri wa kimarekani wanaomiliki baadhi ya vilabu vikubwa vitatu vya England; Manchester United, Liverpool na Arsenal.

Benki kubwa ya Marekani ya JP Morgan itakuwa mdhamini mkuu wa mashindano haya yatakayoshirikisha timu 20, lakini 15 kati ya hizo zitakuwa za kudumu kwa miaka 20 huku 5 zilizobaki zitakuwa zikipanda na kushuka daraja.

Perez anatarajiwa kuwa Rais wa ligi hii, huku wamiliki wa Liverpool, John W. Henry, wa Manchester United, Joel Glazer na wa Arsenal Stan Kroenke, wakiwa makamu wa Rais kwa pamoja.

Mwenyekiti wa Juventus, Andrea Agnelli, atakuwa makamu wa nne wa Rais, nyuma ya wale makamu wa watatu.