- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: URUSI YAKISHAMBULIA KIWANDA CHA NDEGE CHA UKRAINE
Meya wa mji wa Lviv Andriy Sadovyi amesema Uwanja wa ndege wa mji wa Lviv leo umeshambuliwa na makombora ya Urusi wakati ambapo nchi hiyo inapanua kampeni yake ya mashambulizi ya angani kote nchini Ukraine.
Kampeni hiyo ya Urusi imepelekea kuibuka kwa madai ya uhalifu wa kivita na ulengaji wa maksudi wa raia. Meya wa mji wa Lviv Andriy Sadovyi amesema majeshi ya Urusi yamekishambulia kiwanda cha kukarabati ndege kilicho karibu na mpaka wa Poland.
Kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa AFP moshi mkubwa ulionekana ukifuka kutoka katika uwanja huo wa ndege.
Urusi imegeukia mashambulizi ya angani na masafa marefu kutokana na operesheni yao ya nchi kavu kukwama kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Ukraine.