Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 8:39 pm

NEWS: URUSI NA MAREKANI KUKUTANA KUZUIA VITA VYA UKRAINE

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Urusi Vladimir Putin wameridhia kukutana katika hatua za lala salama za kidiplomasia kujaribu kuepusha uwezekano mkubwa wa Urusi kuivamia Ukraine.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ndio masta plan wa mkutano huo, yeye ndie amefanya maandalizi wa kuwakutanisha, Rias Macron amefanya mazungumzo na pande zote mbili kwa njia ya simu. Ofisi ya Macron imesema Biden na Putin wamekubaliana kukutana na baadaye pia wamekubaliana kukutana na pande zote husika katika mgogoro wa Ukraine na Urusi ili kujadili masuala muhimu ya usalama na uthabiti wa Ulaya. Ofisi hiyo imesema mkutano huo utafanyika kwa masharti ya Urusi kutothubutu kuivamia Ukraine.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki amesema nchi yake iko wazi kabisa katika suala hili kwamba wamejitolea kutumia diplomasia hadi pale uvamizi utakapofanyika akisema kwa sasa Urusi inaonekana kuendelea kujitayarisha kuishambulia Ukraine.