Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:26 am

NEWS: UPINZANI WASHINDA KESI DHIDI YA SEREKALI

Arusha. Hukumu ya Kesi ya kupinga mabadiliko ya Sheria mpya ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019 iliyofunguliwa na viongozi wa Upinzani nchini Tanzania katika mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki imetolewa hii leo kwa Vyama hivyo vitano kupewa ushindi na Mahakama hiyo ya Africa.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Maalim Self Sharif Hamad, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa CHAUMA Hashimu Rungwe.

Katika kesi hiyo viongozi hao walikuwa wakiwakilishwa na Mawakili Fatuma Karume, John Mallya na Jebra Kambole

Viongozi hao wa Upinzani wanaomba mahakama hiyo kusitisha kutumika kwa sheria hiyo.

Wanadai kwamba sheria hiyo inakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika masuala ya haki na demokrasia.


Mongoni mwa mapungufu katika shauri hilo ni kuzuia viongozi wa upinzani kutoa elimu ya mpiga kura bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa, kuzuia walinzi binafsi ya vyama na kuingiliwa uhuru wa vyama.