Home | Terms & Conditions | Help

December 3, 2024, 8:34 pm

NEWS: UMOJA WA ULAYA WAZIPA HADHI UKRAINE NA MOLDOVA KUJIUNGA EU

Viongozi wa Umoja wa Ulaya jana Alhamisi wamezipa Ukraine na Moldova 'hadhi ya kuwa wagombea' kujiunga na umoja huo.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya majadiliano baina ya viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa kilele mjini Brussels.

Kupewa hadhi ya kugombea uanachama wa Umoja wa Ulaya ni ishara thabiti ya mshikamano wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Umuzi huo wa viongozi wa Umoja wa Ulaya ni hatua ya kwanza miongoni mwa nyingine nyingi kwa Ukraine na Moldova kujiunga na umoja huo. Hatua hiyo imejiri mnamo wakati Marekani imesema inaipa Ukraine misaada zaidi ya mifumo ya kisasa ya roketi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliupongeza uamuzi huo akisema ni wa kipekee na kihistoria. Hii ni licha ya mataifa hayo wanachama wa zamani wa muungano wa Soviet, kuwa na safari ndefu kabla yajiunge rasmi na kunufaikia faida za kuwa mwanachama ikiwemo soko la pamoja.

"Tumepokea hadhi ya ugombea. Huu ni ushindi wetu. Tumesubiri kwa siku 120 n miaka 30. Tutamshinda adui na tupumzike. Au labda tutaijenga Ukraine upya ndipo tupumzike. Au tushinde, tuijenge nchi upya, tuingie Umoja wa Ulaya kisha tupumzike. Au labda hatutapumzika," amesema Zelensky.