November 22, 2024, 2:21 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UMMY ATAKA MFUKO WA NHIF UBORESHWE.
DODOMA: Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) kuja na mikakati mipya ya kuongeza wanachama pamoja na kuboresha huduma za mfuko huo.
Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo mara baada ya kukutana na Menejimenti ya NHIF na kufanya kikao cha pamoja katika Ofisi za Mfuko huo Jijini Dodoma.
“Ili tuwe na Mfuko endelevu wa Bima ya Afya nchini ni lazima sasa tuwe wabunifu na tuandikishe wananchama wengi hususani ambao sio wagonjwa ili waweze kuchangiana” amesema Waziri Ummy Mwalimu
“Kama tuna Watanzania 10 tumechanga ina maana tunaweza tukamchangia mwenzetu mmoja atakayeumwa baina yetu” amefafanua zaidi Waziri Ummy Mwalimu.