- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UKEREWE WAKAA GIZA KWA ZAIDI YA SIKU 6
Mwanaza: Wakazi wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza wamelilalamikia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wilayani humo kwa kitendo cha kukatika kwa umeme na kukaa giza kwa zaidi ya siku 5 mfululizo huku wakiwa hawaelewi nini hatima yao.
Wananchi hao wameiomba Serekali kuwasaidia kutatua adha hiyo ya Umeme.
Muakilishi imeongea na baadhi ya wakazi wa Ukerewe kujua nini tatizo, mmoja wapo ni Bwana Laurent Babilasi ni Kinyozi katika kata ya Bukindo wilaya Ukerewe Mkoani Mwanza, amesema kuwa "hapa kwetu(Ukerewe) kazi haziendi na tunashindwa kufanya kazi kwasababu umeme haupo kwa zaidi ya siku 6 na kuna baadhi ya maeneo mengine tangu tarehe 2 mwezi huu hakuna umeme, Sasa wafanyakazi na Wanafunzi hawapati huduma ya kunyoa na wametoka likizo ya Pasaka"
"Mimi sijafanya kazi kwa muda sasa na leo nataka nifunge Steshenari yangu kwasababu swala la umeme hapa kwetu nitatizo kubwa, tunaomba Rais Samia atusaidie kwasbabu ili nasisi tuweze kupata riziki ya halali, na tulipe kodi" - Boke Sufaria mkazi wa Ukerewe Mjini
Baada ya kupokea mamalamiko hayo Muakilishi Media ilimtafuta Oparation Meneja wilaya ya Ukerewe Bi Aisha James ili kupata ufafanuzi juu ya Adha hiyo, Aisha amesema kuwa ni kweli wanatatizo hilo la umeme lakini si kwa muda huo kama ambavyo wananchi wanavyoeleza
"Umeme unakuja unakatika, unakaa siku moja then unakuja unakatika tena, na hili nikutokana na changamoto mbali mbali zilizopo katika wilaya yetu kama vile kuchoka kwa nguzo za umeme kwahiyo inasababisha nguzo nyingi kuanguka, changamoto nyingine ni kuungua kwa baadhi ya transfoma kwenye baadhi ya maeneo ya Ukerewe"-amesema Aisha.