Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 12:11 pm

NEWS: UKATILI WA KIJINSIA WAZIMA NDOTO ZA WANAFUNZI.

BAHI: Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Msichana Initiative Rebeca Gyumi amesema toka mwaka 2017 hadi 2018 matukio zaidi ya 404 ya ukatili wa kijinsia yametokea ambapo ndoa za utotoni na ukatili mwingine umepungua kwenye jamii kwa asilimia 64 nchini Tanzania.

Pia Ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa mwaka 2022 inaonyesha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaugharimu uchumi wa dunia kati ya asilimia 3 hadi 8 ya pato lake ambapo nchini Tanzania zaidi ya Billion 6.5 za kimarekani sawa na asilimia saba ya pato la taifa hupotea kutokana na athari zitokanazo na vitendo vya ukatili.


Gyumi ametoa kauli hiyo Desemba 4, 2022, Wilayani Bahi Mkoani Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative.


Gyumi ameendelea kusema kwa sasa kumekuwa na Muamko mkubwa kwa jamii kuripoti Juu ya Vitendo hivyo. ''Lengo letu kama Shirika pamoja na kwamba tunataka kuhamasisha haki za wasichana ukosoma, walindwe na ndoa za utoto , mimba za utoto hatuwezikuleta matokeo chanya kama hatushirikishi jamii,''.


Kwa upande wake Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Mwahamisi Munkunda amewaonya Wenyeviti wa Vijiji Kutoingilia kati kesi yoyote inayohusu ukatili wa Kijinsia huku akiwataka viongozi wa dini,jamii , Wazee wa Kimila kuangalia namna ya kukomesha Vitendo hivyo.


Uwepo wa mila na desturi dumavu na kandamizi kwa wasichana zimechangia kushindwa kuendelea na masomo yao licha ya jitihada za wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kuzuia vitendo hivyo lakini bado vitendo vikiendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku kauli mbiu ya siku 16 zakupinga ukatili wa kijinsia zimebeba ujumbe wa Msichana Mwenye Ndoto Ni Moto.

Nao baadhi ya waadhirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo wamesema vitendo hivyo vimewaadhiri afya ya akili nakuwaharibia ndoto zao, huku mmoja wa waathirika ambaye alifanikiwa kuokolewa na wasamalia wema akisema haikua rahisi kuwakwepa wahalifu wa utekelezaji wa vitendo hivyo.