Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 9:43 am

NEWS: UKATILI TISHIO CHAMWINO,UKEKETAJI UKITAJWA.

DODOMA: Takwimu za mwaka 2020 zinaonyesha watu 439 walifanyiwa ukatili katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma na Kijiji cha Nzali Kata ya Chilonwa wako 16 huku 89 waliochini ya miaka 19 wamekeketwa kijijini hapo.

Wakati huo huo Kati ya wajawazaito 14,900 waliojifungua katika kipindi ya mwaka 2020 wilayani hapo 3,438 ni wasichana waliokuwa katika umri wa chini ya miaka 18.

Takwimu hizo zimetolewa na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na watoto wilaya ya Chamwino Neema Mlula, wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Iringa Mvumi na Nzali kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya hiyo bado vipo kwa wingi hali ambayo inahitaji jitihada za makusudi kuvikabili.

“Ukatili mwingi unafanyika nyumbani wanafamilia ndiyo tunakuwa wakwanza kulindana,watoto wetu wanarawitiwa katika nyumba zetu lakini tunaogopa kusema kwa kuona aibu”amesema

Hata hivyo, amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo bado vimeshika kasi katika wilaya hiyo ni mimba za utotoni na ndoa katika umri mdogo.

Amesema, watoto wengi wanapata ujauzito katika umri mdogo na kushindwa kumaliza masomo yao lakini watuhumiwa hawachukuliwi hatua kutokana na kulindana.

“Mimi kama nilivyosema hapo awali ni mratibu wa masuala ya afya ya uzazi na watoto hivyo nafahamu katika wilaya yetu namna ambavyo hali ilivyo wasichana wengi wanakuja kujifungua wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 lakini wengine tayari wameshaolewa katika umri kama huo na kuacha masomo”ameisisitiza

Naye mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Shida Hamisi, amesema moja ya sababu ambazo zinachangia kuongezeka kwa ndoa nyingi za utotoni ni viongozi wa dini kushiriki katika kufungisha ndoa bila kuhoji umri wa wanandoa.

“Kuna ndoa moja tulishuhudia sitataja kanisa kuna binti alikuwa anaoelewa kimuonekanao tuu anaonyesha ni mtoto mdogo anaolewa na baba mtumzima lakini mchungaji wala hakuohoji na kuendelea kufungisha ndoa ile”amesema

Kutokana na hali hiyo amewaomba viongozi wa dini kuhakikisha kuwa kila wanapofungisha ndoa wapate vyeti vya kuzaliwa vya wanandoa.

Askari dawati la Jinsia wa Wilaya hiyo Nabwike Wilson amesema Kesi nyingi chanzo ni wazazi kutokuwa karibu na watoto wao na ikitokea wanamaliza kimila.

“Niwaombe Watoto waepuke lifti na wazazi watoe ushidi mahakamani, tunaomba Msituharibie ushahidi utakuta mtoto kafanyiwa ukatili wa kingono baada ya siku tatu ndo mnamleta polisi baada ya kushindwa kumalizana tayari mmeshamwogesha tunakosa ushahidi,”amesema Wilson.

Afisa kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Florence Chaki, ametoa wito kwa wakazi wa kijiji hicho kujitokeza kutoa malalamiko yao pindi wanapoona haki yao inapotea.

“Tume milango yake ipo wazi kama mnaona kunashida ambayo inasababisha kupoteza haki yenu njooni msikae kimya nakusema tuu namwachia mungu pambaneni kupata haki yenu na sisi tutawasaidia”amesema Chaki.

Maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga kukatili wa jinsia yanafanyika katika wilaya hiyo kwa kuratibiwa na shirika Action Aid Tanzania.