- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UKATILI BADO KIZUNGUMKUTI SINGIDA.
SINGIDA: Kati ya kesi saba zilizoripotiwa mwaka 2020 Wilaya ya Singida Mjini, kesi tatu zikikuwa za ubakaji wakati nne ni ndoa za utotoni huku Afisa ustawi wa jamii Raphael Tilihongelwa akisema takwimu hizo haziendani na uhalisia katika wilaya.
Tilihongelwa ametoa takwimu hizo katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili katika mkutano ulioandaliwa na mashirika ya ActionAid na Afnet Kijiji cha Mnkola.
Amesema Ripoti iliyotolewa haimanishi matukio ya ukatli kwa watoto hasa wakike hayapo yapo kwa kiasi kikubwa isipokuwa jamii imekuwa ikifumbia macho matukio mbalimbali yanayotokea nakuwataka vijana kuchukua tahadhari na kuepuka kufanya ngono katika umri mdogo ili kuziepusha familia zao na madhara yanawoweza kutokea.
''Nawakati mwingine mtoto anaweza kufanyiwa vitendo vya ukatili lakini jamii ikakaa kimya kwa madai ya kulinda uhusiano wao, Wakati mwingine kesi zinazofika mahakamani zinacheleweshwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na kukosekana kwa ushirikiano baina ya pande mbili ,''Amesema Tilihongelwa.
Mbali na hayo amewataka Wamama kutoruhusu watoto wao kukeketwa kwani kufanya hivyo kunamwondolea hamu ya kufanya tendo la ndoa huku akiwataka kutoa taarifa jeshi la polisi pindi inapotokea vitendo hivyo.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Singida Dc Walter Jonael amesema kutokana na takwimu nyingi za Singida kuonyesha waliopo shuleni wengi ni Wasichana ni jukumu la wazazi kujitathimini kama wanatimiza wajibu wao ipasavyo ili kupunguza wimbi la tatizo hilo huku akisisitiza ipo shida ya Usimaminzi kwa wazazi hali inayopelekea watoto kuingia kwenye vishawishi nahuo ni unyanyasaji.
''Wanawake wanapata ukatili wakutosha wakiwa njiani pindi wanapotoka shule na kurejea nyumbani,Watoto hawana ulinzi kabisa wazazi hawalindi watoto, kwa sababu vipo viashiria na pia kuna ukweli kwamba unaona mtoto wakike mdogo amesimama na mvulana lakini unapita unajifanya hauoni , hiyo tabia ikiendelea kwa muda mrefu yule mtoto hawezi kuwa na mawazo ya kuendelea kusoma na wengi kushindwa kumaliza shule kwa sababu ya vijana wa bodaboda kuwadanganya na vitu vidogovidogo kama vichipisi,'' Amesema Jonael.
Mkurugenzi wa Shirika la AFNET Joy Njelango amewataka Wazazi kuandaa utaratibu mzuri wa watoto kupata chakula mashuleni lengo kuwaepusha na vishawishi njiani pindi wanapotoka muda mbovu shuleni.
''Watoto wanarudi mchana kwenda kula chakula nawanatembea mwendo mrefu kwanini wazazi kinashindikana nini kile chakula unachomwekea mtoto kisiletwe shuleni, mbona kunapokuwa na kambi za darasa la saba hilo linawezekana, kwanini lisiwe endelevu ili watoto wasome muda wote halafu warudi tu nyumbani,Tuna mikutano yetu makanisani suala la maadili hatungoji mpaka siku ya wadau kuja kusema,''amesema Njelango.