Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:45 am

NEWS: UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA

Waziri wa usafirishaji nchini Uingereza Grant Shapps amepiga marufuku abiria wote kutoka nchini Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzuia maambukizi aina mpya ya virusi vya corona.

"Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika mataifa ya Irish kuanzia saa kumi alfajiri," amesema Grant Shapps, waziri wa usafirishaji nchini Uingereza.

Kuanzia tarehe 22 Januari, saa kumi alfajiri wasafiri wote wamepita nchini Tanzania ndani ya siku 10 hawataruhusiwi kuingia Uingereza na mataifa ya Irish, na wale ambao wana haki ya makazi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kujitenga nyumbani kwao watakapowasili.