- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UHOLANZI KUISHTAKI URUSI KWA KUDUNGUA NDEGE YA MALAYSIA
Serekali ya Uholanzi imesema kuwa imepanga kuishtaki Urusi katika mahakama ya Ulaya kuhusu haki za binadamu ya ECHR kwa hatua yake ya kuidungua ndege ya shirika la ndege la Malaysia mwaka 2014.
Ndugu na Jamaa wa wahanga 65 wa Uholanzi waliofariki kwenye ajali ya ndege waliwasilisha malalamiko yao kwenye mahakama hiyo yenye makao yake mjini Strasbourg, wakiitaka Urusi kubeba dhamana ya tukio hilo ambamo watu wote waliokuwa kwenye hiyo waliuawa.
Uholanzi na Australia zimesema zinaibebesha jukumu Urusi kwa kuidungua ndege hiyo, iliyokuwa safarini kuelekea Kuala Lumpur kutoka Amsterdam.Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi Stef Blok amesema upatikanaji wa haki kwa wahanga 298 wa ndege hiyo iliyokuwa na nambari za safari MH17, utaendelea kuwa kipaumbele cha juu kabisaa cha serikali yake.