- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UGANDA YAIDHINISHA MATUMIZI YA KISWAHILI
Bazara la mawaziri nchini Uganda, limeidhinisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kutumika nchini humo mbali na lugha ya kingereza.
Bazara hilo katika maamuzi yake limekubali kutekelezwa kwa mapendekezo ya azimio la 21 l viongozi wa Jumuiya ya Africa mshariki, yalioidhinisha matumizi ya lugha ya kiswahili kutumika kanda hii, na sasa itakuwa lazima kwa shule za upili na msingi kufunza lugha ya kiswahili nchini Uganda.
Lugha ya kiswahili nchini Uganda kwa muda mrefu imekosa kutumika na raia wengi, kinyume na hali ilivyo katika mataifa jirani ya Kenya, Tanzania, Burundi na hata DRC, kutokana na kile raia wengi wamekuwa wakihusisha lugha hiyo na maafisa wa usalama ambao miaka ya zamani walitumia lugha hiyo kuwanyanyasa raia, hatua iliochangia raia kuogopa lugha idhimu ya Kiswahili.
Hatua hii ya Uganda inajiri siku moja tu kabla ya dunia kuadimisha siku ya kimataifa ya Lugha ya kiswahili Julai 7, siku iliotambuliwa baada ya umoja wa mataifa kutambua lugha ya kiswahili .