Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:51 pm

NEWS: TWITTER YAJIPIMA UBAVU KUINUNUA TIK TOK

Kampuni ya Twitter Inc ya nchini Marekani imesema imewasiliana na mmiliki wa TikTok Bw. Bytedance kwa lengo la kutaka kuinunua operesheni za mtandao huo kwa nchini Marekani.

twitter inataka kununua mtandao wa Tik tok licha ya kuwa thamani ya mtaji wake kwenye soko la hisa ni sawa na Tik tok.

Kwasasa twitter inamtaji wa Dola za Marekani Bilioni 30 sawa na rasilimali za mtandao wa tik tok.

Hata hivyo hakuna uthibitisho wowote iwapo Twitter itaweza kununua na kuipiku kampuni ya Microsoft Corp na kuweza kukamilisha ununuzi huo katika siku 45 Rais wa Marekani Donald Trump alizowapa ByteDance kufikia makubaliano ya kuuza kampuni hiyo, chanzo kimeeleza Jumamosi.

Taarifa za Twitter na TikTok kuwa katika mchakato wa awali za mazungumzo na Microsoft ikionekana kama inaongoza katika manunuzi hayo ya programu hiyo ya TikTok inayoendeshwa Marekani iliripotiwa hapo awali na jarida la The Wall Street.

“Twitter itakabiliwa na wakati mgumu kuweza kukusanya fedha za kutosha kununua mtandao wa TikTok unaoendesha shughuli zake Marekani. Haina uwezo wa kukopa kiasi cha kutosha,” amesema Erik Gordon, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Michigan.

“Iwapo Twitter itajaribu kukusanya kikundi cha wawekezaji, masharti yatakuwa magumu. Wadau wake wanaomiliki hisa wanaweza kupendelea uongozi uweke mkazo na uangalizi zaidi katika biashara ambayo tayari wanayo.