- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUME YA UCHAGUZI YAMPITISHA LISSU MGOMBEA URAIS CHADEMA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imempitisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema Tundu Lissu kupeperusha bendera ya chama chake katika Uchaguzi Mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu.
Taarifa ya kupitisha kwake imetolewa hii leo Agosti 25, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya taifa Uchaguzi Jaji Rufaa Mstaafu Semistocles Kaijage kupitia televishemi ya Taifa TBC.
leo Agosti 25, 2020, lilikuwa ndio hitimisho kwa zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za uteuzi kwa nafasi za Ubunge, Udiwani na Urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), lililoanza Agosti 5, 2020, ambapo takribani vyama 17 vyenye usajili wa kudumu na vyenye sifa vilisimamisha wagombea wa Kiti cha Urais.
Wagombea wengine waliopitishwa na NEC hii leo, ni pamoja na John Mgufuli kupitia CCM, Hashim Rungwe kupitia CHAUMMA, Bernard Mende kupitia ACT Wazalendo, John Shibuda kupitia chama cha ADA-TADEA, Khalfan Mohamed Mazurui kupitia chama cha UMD, Leopold Mahona kupitia chama cha NRA.
Wengine ni Seif Maalim Seif wa chama cha AAFP, Queen Cuthberta Sendiga kupitia chama cha ADC, Philipo John Fumbo wa chama cha DP, Profesa Ibrahim Lipumba kupitia CUF, huku mgombea wa chama cha CCK na chama cha NLD wakikatwa kwa kushindwa kutimiza vigezo vya NEC