Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:40 am

NEWS: TUME YA UCHAGUZI YAJIBU VIKWAZO VYA MAREKANI

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC), Jaji Semistocles Kaijage amesema taarifa ya vikwazo iliyotolewa na Marekani Juu ya watu walioharibu Uchaguzi Mkuu wa Octoba 2020 haijafafanua kinacholalamikiwa "na sheria za Tanzania zinaelekeza kupeleka mashitaka mahakamani pale mlalamikaji anapoona sheria hazikufuatwa"

Jaji Kaijage ameitaka Marekani kutoa ufafanuzi zaidi ya namna gani uchaguzi mkuu wa Tanzania ulivyoigiliwa.

“Hayo ni maoni yao, sasa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi atafanya nini? Waeleze basi huo uchaguzi uliingiliwaje? Maelezo yao hayajaeleweka bado,” alisema.

Jaji Kaijage amenukuliwa Jana na Gazeti la kila siku la habari la Mwananchi akisema kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na waangalizi wa uchaguzi na walitoa ripoti zao za awali na wameendelea kutoa ripoti kuu mpaka sasa.

“Kulikuwa na accredited observers (waangalizi waliopewa vibali) na walitoa ripoti. Tuone walisemaje kwenye ripoti zao. Kama Marekani walikuwa na waangalizi ripoti yao itaonyesha. Kwa sasa mimi niko likizo sijaona ripoti walizotoa.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alitangazwa mshindi na Tume hiyo na kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano Octoba 30, 2020

Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa na Mpinzani wake Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

Jaji Kaijage anasema kuwa ; “Unaposema uchaguzi umeingiliwa inakuwa ni general statement kauli ya jumla). Ni lazima useme umeingiliwa kivipi? sio sweeping statement. Sheria zetu ziko wazi kama unaona kuna kasoro baada ya uchaguzi unafanya uchunguzi wa kisheria uone kama kuna makosa labda katika uteuzi wa wagombea au wakati wa kupiga kura. Baada ya hapo unakwenda mahakamani kushitaki.”

Alipoulizwa kuhusu vikwazo hivyo alisema: “Issue sio mara ya kwanza au ya pili kuwekewa vikwazo, ila ni basis (msingi) ya hivyo vikwazo. Aulizwe yeye aliyechukua hatua na sio sisi. Lakini statement yao iko too general, haiko concrete.”

Katika tovuti ya Serikali ya Marekani umetolewa ufafanuzi wa kauli ya Pompeo ikisema vitendo vilivyofanywa na maofisa wanaotuhumiwa ni mwendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia.

“Waangalizi wa uchaguzi na asasi za kiraia zilishuhudia ukandamizaji na uvunjifu wa haki za binadamu, kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Wagombea wa upinzani walienguliwa, wananyanyaswa na kukamatwa.

“Kuongezeka kwa kasoro za upigaji kura, kufungwa kwa intaneti, manyanyaso kwa waandishi wa habari na vurugu zilizosababishwa na vyombo vya usalama vyote viliufanya uchaguzi huo usiwe huru wala wa haki. Viongozi wa asasi za kiraia walipata vitisho na wa upinzani wamekimbia nchi wakihofia usalama wao,” imesema taarifa hiyo.

Marekani imeitaka Serikali ya Tanzania kuchunguza na kuwachukulia hatua waliohusika na makosa ya uchaguzi na vurugu.

Marekani imekuwa na Utamaduni wa kila siku wa kuiwekea vikwazo au kumuwekea mtu fulani vikwazo pale ambapo inapoona kuwa kunauvunjwaji wa haki za kiraia na utawala bora katika nchi fulani.

Hivi karibuni mwaka jana Wizara ya mambo ya njee ya Marekani ilitangaza kumuwekea vikwazo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania Paul Makonda kwa kile walichodai kuwa alishiriki kwenye mambo mengi yalikuwa yanahatarisha haki za kirai na utawala bora.