Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:19 pm

NEWS: TRUMP AIDHININISHA MPANGO WA KUWAONDOA WANAJESHI WA MAREKANI

Rais wa tAIFA la Marekani Bw. Donald Trump hatimaye ameidhinisha mpango wa kuwaondoa askari 9,500 wa Kimarekani kutoka nchini Ujerumani, baada ya waziri wa ulinzi Mark Esper kuwasilisha mpango huo siku ya Jumatatu.

Trump confirms plans to pull some US troops out of Germany

Trump alitangaza mwezi Juni kwamba atapunguza askari wa Marekani walioko Ujerumani, kwa madai kuwa Berlin haiwajibiki ipasavyo katika mchango wake kwenye Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO.

Kundi la maseneta kutoka vyama vyote lilitangaza juhudi za kumzuia Trump, na kubainisha marekebisho ya sheria katika matumizi ya ulinzi kwa mwaka 2021, hadi pale waziri wa ulinzi atakapowasilisha ripoti ya kuthibitisha kwamba hatua ya kuwaondoa askari haitiishii usalama wa nchi na washirika wake. Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon inasema ikiwa zoezi hilo litatakelezwa, baadhi ya askari watapelekwa katika kundi la nchi za mashariki kama ishara ya kutuma ujumbe kwa Urusi.