- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRA YAZIFUNGULIA AKAUTI ZOTE ZA WAFANYABIASHA ZILIZOFUNGWA
Morogoro. Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara zilizokuwa zimeshikiliwa na mamlaka hiyo kutokana na madeni ya kodi kipindi cha utawala wa Rais John Magufuli.
Taarifa hiyo imetolewa leo hii May 21, 2021 na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF) lililofanyika mjini Morogoro.
Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum. Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.
Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.
"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo "Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo