- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TOZO ZA SIMU KUFANYIWA MAREKEBISHO UPYA.
Serekali ya Tanzania imesema kuwa imesikia malalamiko ya Watanzania Juu ya Tozo mpya za Sim, na kwasasa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameshaitisha kikao cha kufanya mapitia juu ya tozo hizo.
“Kwa sababu hii ni sheria ya Bunge, na tayari imeshapitishwa na inatakiwa kutekelezwa, lakini kuna maeneo ambayo yanaangukia kwenye kanuni ambazo zinaangukia Wizara ya Fedha na Wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano.”
Kauli ya Waziri Nchemba imekuja siku chache mara baada ya Wadau na wanaharakati mbalimbali nchini kupaza sauti wakilalamikia juu ya hatua ya serekali kuongeza tozo kubwa kwenye miamala ya simu.
“Nitoe rai kwa wananchi kuwa Serikali imesikia malalamiko ya wananchi na tayari tumeendelea kuyafanyia kazi, Waziri Mkuu ameshaitisha kikao kesho kuendelea kupitia masuala haya haya.” – Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Julai 19, akitoa taarifa ya miamala ya simu.
"Tumeshawaelekeza wataalam wetu waangalie kipengele kinachozungumzia masuala ya National Payment System ambayo inaongelea masuala ya miamala na Electronic and Postal Communication. Timu za wataalam pamoja na sisi tutaendelea kuyafanyia kazi." - Waziri Mwigulu Nchemba
Kwa upande wake Waziri wa Mawasilino na teknolojia ya habari Sr. Faustine Ndugulile amesema kwamba wao kama Wizara husika wameanza kukusanya maoni juu ya ongezeko la tozo hizo za simu.
“Sisi kama Sekta ambayo imeguswa na tozo hii tunakusanya maoni ushauri na kuchakata takwimu na Wizara yangu itakupa ushirikiano Waziri Nchemba ili maelekezo ya Viongozi wetu tuhakikishe yamefanywa, niwaombe Watanzania tuwe watulivu” amesema Waziri Ndugulile
Kutokana na pendekezo la tozo hiyo ambayo Serikali imekuwa akisisitiza kuwa kodi ya mshikamano kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, hivi karibuni Serikali imetoa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa makato hayo ambayo huenda nayo yakaleta kilele miongoni mwa watumiaji.
Kanuni zilizopelekwa kwa watoa huduma za simu kwa ajili ya kuanza utekelezaji ifikapo Agosti mosi zinaonyesha kuwa kila laini ya simu itatozwa Sh5 pindi itakapoongezewa salio lisilozidi Sh1,000 na itatozwa Sh223 kwa kuongeza salio linalozidi Sh100,000.
Kwa anayeongeza salio la Sh1,001 hadi Sh2,500 atatozwa Sh10, Salio la Sh2,501 hadi Sh5,000 tozo mpya ni Sh21, Salio la Sh5,001 hadi Sh7,500 tozo mpya ni Sh40, salio la Sh7,501 hadi Sh10,000 tozo mpya Sh76, Salio la Sh10,001 hadi Sh25,000 tozo mpya Sh113, salio la Sh25,001 hadi Sh50,000 tozo mpya Sh153 na salio la Sh50,001 hadi Sh100,000 tozo itakuwa Sh186.