Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:57 pm

NEWS: TOZO ZA MIAMALA YA SIMU ZAPUNGUZWA KWA ASILIMIA 40%

Habari Jema kwa watumiaji wa mitandao ya simu nchini ni kwamba kuanzia kesho Septemba 1, 2021 Serekali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba Leo August 31,2021 ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021 na kupunguza viwango vya tozo za miamala kwa asilimia 30%.

Mwigulu amesema kuwa hatua hiyo ni kutokana na utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hasaani ambaye alielekeza tozo zipitiwe upya baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu tozo hizo.

Serikali pia imefanya majadiliano na watoa huduma za simu ambao na wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza katika miamala ya kutuma na kutoa fedha kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%.

Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa Tangazo la Serikali kesho September 01,2021 ambapo Serikali imesema inaamini uamuzi huo utatoa nafuu kwa Wananchi na kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyokusudiwa wakati tozo hizo ziliporidhiwa na kupitishwa na Bunge la Bajeti la Mwaka 2021/2022.

Tangu kuanza kwa tuzo hizo mpya za miamala ya simu kuwa na malalamiko makubwa kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa simu