- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TITO MAGOTI NA MWENZAKE WAACHILIWA HURU
Dar es salaam. Hatimaye Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemuachia huru Afisa wa Kituo cha Sheria na haki za binaadamu cha Tito Magoti na mwenzake Theodory Giyan mara baada ya kukubali kuilipa serekali Tsh. Milioni 17.3 baada ya kupatikana na hatia ya kuongoza genge la uhalifu.
Wawili hao walikamatwa Disemba 2019 na kufunguliwa mashitaka matatu ya uhujumu uchumi ikiwemo utakatishaji fedha. Kesi yao iliahirishwa mara 26 kabla ya kuingia makubaliano na mwendesha mashitaka mnamo Januari 5, 2021.
Hukumu hiyo imetolewa leo, Januari 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Mtega, baada ya washtakiwa hao kukiri mashtaka yao kwa DPP.
Mbali na kulipa fidia, mahakama hiyo, imewahukumu adhabu ya kutokutenda kosa lolote la jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia leo.
Hakimu Mtega alisema, mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao kwa kosa la kuongoza gengea uhalifu.
"Washtakiwa mmetiwa hatiani kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu wa kupangwa, hivyo mnatakiwa kulipa kiasi cha Sh 17, 354,535 kama fidia kwa Serikali," alisema Hakimu Mtega.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka washtakiwa kati ya Februari mosi na Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam na katika maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi Tanzania, mshtakiwa Magoti, Giyani na wenzao ambao hawajafikishwa mahakamani, walishiriki makosa ya uhalifu wa kupanga kwa kumiliki programu za kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kufanya uhalifu na kupelekea kujipatia fedha kiasi cha Sh 17, 354,535