- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TIMU 20 UWANJANI,MTATURU JIMBO CUP.
SINGIDA: Naibu Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Pauline Gekul Octoba 15,anatarajiwa kuzindua ligi ya Mtaturu Jimbo Cup inayotarajiwa kutimua vumbi katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi,Mkoani Singida ikishirikisha timu 20.
Ligi hiyo itasindikizwa na burudani kutoka kwa msanii wa miondoko ya Singeli mzee wa Bwax.
Akizungumza na mtandao huu Octoba 13,Msemaji wa Kamati ya Uratibu wa Ligi ya Mbunge Yahya Njiku amesema ligi hiyo itachezwa katika Tarafa zote za Ikungi na Mungaa ambapo timu zitakazoshiriki zinatoka kwenye Kata 13 zilizopoJimbo la Singida Mashariki.
“Ligi hii imeanzia ngazi ya vijiji na sasa imefikia ngazi ya jimbo,siku ya uzinduzi kutakuwa na mechi ya utangulizi kati ya watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Ikungi,lakini mechi ya ufunguzi ya ligi itachezwa kati ya Kikio na Sokoni,”amesema.
Ametaja timu nyingine zitakazoshiriki ligi hiyo kuwa ni pamoja na Sambaru,Mkiwa,Ghorofani,
Ametaja lengo la ligi hiyo kuwa ni kuibua vipaji,kuhamasisha vijana kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa burudani kwa wachezaji na washangiliaji.
“Kama mnavyojua Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa chachu kwa vijana kushiriki katika mambo ya michezo na shughuli nyingine,hivyo nasi tumetumia dhamira hiyo kuwakusanya pamoja ili wapate nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,”alibainisha.
Kwa upande wake Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambaye ndie muandaaji wa ligi hiyo amesema ameamua kuwakutanisha vijana pamoja ili watumie michezo hiyo kutengeneza ajira na kujiimarisha kiafya ili wakitoka hapo wawe wamechangamka kuweza kuendelea na kufanya shughuli za kulijenga Taifa.
“Kama tunavyojua michezo ni furaha,michezo ni amani,ukiwa na furaha na amani hakuna kitu utafanya kitashindwa kufanikiwa,tunaelekea msimu wa kilimo,vijana wanatakiwa wakafanye kazi,tunatarajia mchezo huu utatengeneza mwanya mkubwa wa vijana kuimarisha afya zao,hivyo baada ya ligi hii kituo kinachofuata ni shambani,”alisema Mtaturu.