- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TFF YAOMBA RADHI KUHAIRISHWA MECHI YA SIMBA VS YANGA
Dar es Salaam. Shirikisho la kabumbu Tanzania (TFF) limeomba radhi kwa wadau wa soka wote nchini kufuatia kitendo cha kuahirishwa kwa mechi baina ya Simba na Yanga, huku ikiielekeza Bodi ya Ligi kutoa taarifa ya kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo jana May 8, 2021.
Shirikisho hilo Jana Jumamosi liilazimika kusogeza muda wa mechi mbele katika mechi ya ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga na Baadaye, Bodi ya Ligi ilitangaza kuahirisha kwa mchezo huo uliikuwa umepangwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo Jumapili Mei 9, 2021, imeeleza kuomba radhi wadau wa soka na kutoa maelekezo kwa Bodi ya Ligi itoe taarifa ya kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo sambamba na kushughulikia viingilio vilivyolipwa na mashabiki na wadau wa soka.
“Tunawaomba wapenzi wa mpira kuwa watulivu wakati jambo hili linashughulikiwa kwa haraka kwa taratibu za kikanuni, lakini huku tukishirikiana kwa karibu na wadau wote ikiwemo Serikali,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa jambo hilo linaendelea kushughulikiwa kikanuni, kufanya vikao mbalimbali, pia itakutana na klabu hizo mbili Simba na Yanga.
SABABU YA KUHAIRISHWA KWA MECHI.
Jana muda mchache mara baada ya TFF kutoa taarifa ya kusogezwa kwa muda wa mchezo huo kutoka saa 11 jioni na kuupeleka mpaka saa 1 usiku, wanajangwani Club ya Dar Young Africa waligomea mabadiliko hayo huku wakitoa sababu ya kugomea muda huo kwakuwa mabadiliko hayo yalikuwa yanakwenda kinyume na kanuni ya 15 inayohusu taratibu za mchezo ambayo inasema mabadiliko yoyote ya muda wa mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande husika angalau saa 24 kabla ya mchezo husika.
Mara baada taarifa hiyo, Club hiyo ilipeleka timu uwanjani muda uliokuwa umepangwa hapo awali wa saa 11 na kufanya mazoezi ya kupasha mweli ya kujiandaa na mechi ( warm up) baada ya dakika kadhaa wakatoka uwanjani na kurudi kambini.
Nayo kwa upande wa Wekundu wa Msimbazi Simba walikwenda uwanjani kwa muda uliofanyiwa mabadiliko na baadae na wao wakaondoka, baada ya sintofaham yote hiyo ndio Bodi ya Ligi ikalazimika kuhairisha mchezo huo.