- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TCRA YAIPIGA FAINI YA BILIONI 11 KAMPUNI YA INTERNET
Dar es salaam. MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga Faini ya Sh.bilioni 11.89 Kampuni ya Raha Limited watoa huduma ya Internet kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutumia masafa ya mawasiliano ya Radio katika wigo 1452-1482 MHZ bila kuwa na leseni halali kutoka TCRA tangu 24 Machi 2020.
Taarifa hoyo imetolewa hii leo Agosti 28, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi James Kilaba Jijini Dar es salaam.
Kilaba amesema kuwa TCRA ilitoa leseni ya matumizi ya huduma za mawasiliano kimkoa, Leseni ya miundombinu ya mawasiliano, Leseni ya Kitaifa ya matumizi ya mawasiliano ya kieletroniki, leseni ya kufunga na kutengeneza vifaa vya Mawasiliano na Leseni ya matumizi ya namba kwa muda tofauti tofauti.
Mhandisi Kilaba amesema kampuni ya Raha baada ya kupata leseni walitakiwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa kujenga,kusimika, kutunza ,kutumia na kusimamia miundombinu ya mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Tanga ifikapo Februari 2020 na Kilimanjaro ifikapo Septemba 2021 pamoja na kuandaa na kuwasiliasha mpango wa kuendeleza rasilimali Watu kwa Mamlaka hiyo.
Amesema kuwa katika kufanya kazi waliweza kuchukua masafa ya mawasiliano ya Radio mkoani Mtwara bila kubali na kupigwa faini sh.Bilioni 11.85.
Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Kilaba amesema kampuni Raha wanatakiwa kulipa faini sh.milioni 10 kwa kujenga Miundombinu ya mfumo wa mawasiliano kuendesha na kutoa huduma za mawasiliano mkoani Mtwara bila ya kuwa na Leseni kutoka TCRA, Kulipaa Faini ya Sh.milioni 5 kwa kutotimiza masharti ya Leseni baada ya kushindwa kutoa huduma mkoani Kagera Agasti 2019.
Aidha amesema kampuni hiyo inatakiwa kulipa sh.milioni 5 kushindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa mahesabu ya ndani ya miezi sita kuanzia mwaka wa hesabu na sh.milioni tano zingine ni kushindwa kuwasilisha mpango mkakati wa kuendeleza rasilimali Watu huku faini nyingi sh.milioni 10 kushindwa kutimiza masharti ya leseni husani kushindwa kuomba upya kwa nuda uliopangwa