- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TCRA WAIFUNGIA CHANELI YA HUMPHREY POLEPOLE
Dar es saalm. Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekisimamisha kwa muda Kipindi cha Shule ya Uongozi cha online TV kinachorushwa na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole.
Kamati hiyo imefafanua kwambaHumphrey Polepole Online Television ina mapungufu ya kutokuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi na utangazaji wa habari, jambo linalowapelekea kukiuka sheria, kanuni, misingi na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari katika kazi zao.
Aidha TCRA imetoa Onyo Kali kwa Kituo cha Humphrey Polepole Online Television na imemtaka mmiliki wa Kituo hicho kuhakikisha kituo hicho kinakuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji ili kuleta ufanisi na tija Katika vipindi, pia Kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha vipindi vyake vyote vinazingatia sheria, kanuni, misingi na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari pamoja na masharti ya leseni yake na baada ya kufanyia kazi Maelekezo hayo Kituo hicho kinatakiwa kutoa taarifa kwa TCRA
Pia, TCRA imesema kuwa ikijiridhisha kuwa Maelekezo yaliyotolewa yametekelezwa Kipindi cha Shule ya Uongozi kitarejea na kitakuwa chini ya uangalizi wa TCRA kwa Kipindi cha miezi 6.