- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TANZANIA YAPOTEZA ZAIDI YA TRILIONI 153 KATIKA MAPATO NDANI YA MIAKA 9.
DODOMA: Ikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa bunge la bajeti la mwaka wa fedha 2022/ 2023 Wadau wa Maendeleo wameitaka Serikali kuziba mianya iliyopo katika ukusanyaji wa Kodi nchini.
Wamesema, nchi imekuwa ikipata hasara ya zaidi ya Tsh. trilioni 17.4 kila mwaka, kuanzia mwaka 2013 hadi sasa kwa sababu ya kuwepo mianya hiyo katika makusanyo ya mapato.
Wamesema mianya hiyo ni pamoja na ucheleweshaji wa utatuzi wa Migogoro ya ulipaji kodi,ufuatiliaji mdogo kwa watoza kodi na matumizi madogo ya teknolojia kwa serikali za mitaa.
Nyingine ni kutolipa malimbikizo ya kodi, kutofuata sheria ipasavyo kwa mamlaka za umma, uchumi usio rasmi pamoja na mamlaka za umma kutotilia mkazo utoaji wa risiti za mashine za (EFD) .
Wadau hao wametoa maoni yao leo wakati wa kikao maalum kilichowakutanisha wadau wa elimu, maendeleo ya jamii, uchumi na maofisa mipango kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.
Mkutano huo ulifanyika Jijini Dodoma chini ya ufadhili wa shirika la Action Aid Tanzania, lengo ikiwa kutoa mapendekezo njia zitakazotumika kuboresha mgao wa bajeti kwa sekta muhimu ili kupunguza changamoto kwenye Sekta hiyo.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti maalum uliofanywa kwa ufadhili wa shirika la Action Aid Tanzania kwa kushirikiana na taasisi na wizara mbalimbali za umma, Mshauri wa Ushuru kutoka Action Aid Tanzania, Dkt. Balozi Morwa, amebainisha kuwa asilimia 20 tu ya makadirio ya mapato yaliyopotea Kwa kipindi cha mwaka 2019/20, ambayo yalikuwa Dola za Kimarekani bilioni 1.9, sawa na Shilingi Trilioni 3.4 ingeweza kuwalipa walimu 186,898 wa shule za awali na msingi, gharama za kusomesha watoto wote milioni 3.5 wanaokadiriwa kukosa shule, pamoja na ujenzi wa vyumba vyote vya kulala 226,065 vinavyohitajika, miongoni mwa mengine.
Morwa amesema “Kutokana na matokeo hayo, ni jambo la busara kwa serikali, watunga sera na mamlaka zinazohusika na waangalizi kuongeza juhudi za pamoja ili kusaidia kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya ukusanyaji wa mapato nchini ili kuchochea maendeleo yanayohitajika kote nchini,” .
"Kuna haja ya serikali kuanza kufanya uchambuzi wenye tija katika kubainisha na kuweka vipaumbele vya sekta ambazo zinapaswa kupokea fedha kubwa," ameongeza.
Akipokea mapendekezo hayo katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Asante Rabi Sangenoi, amewapongeza wadau hao kwa uwasilishaji huo kwa wakati, na kubainisha kuwa serikali, kuanzia ngazi ya taifa hadi mkoa itafanya kazi ya kutatua kero hizo.
"Serikali daima imekuwa ikifurahishwa na michango mizuri na msaada kutoka kwa washirika wa maendeleo, ikiwa ni pamoja na Action Aid," amesema
Katika mada yao ya jumla wakati wa mkutano huo, wadau wengine wameipa serikali jukumu la kuhakikisha inaongeza mgao wa bajeti kwa sekta ya elimu, angalau kuzingatia Mfumo wa Utekelezaji wa Dakar - Elimu kwa Wote.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Action Aid Tanzania , Joram Wimmo amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali na wananchi ili kusukuma mbele uboreshaji wa sekta muhimu za kijamii na kiuchumi ndani ya wilaya hiyo na katika maeneo mengine ya nchi.
Mnamo Aprili 2000 zaidi ya washiriki 1,100 kutoka nchi 164, ikiwa ni pamoja na Tanzania, walikusanyika Dakar, Senegal, kwenye Jukwaa la Elimu Duniani, kuanzia walimu hadi mawaziri wakuu, wasomi, watunga sera, mashirika yasiyo ya kiserikali hadi wakuu wa mashirika makubwa ya kimataifa. ilipitisha Mfumo wa Utekelezaji wa Dakar, Elimu kwa Wote.
Mfumo huo, miongoni mwa mengine, ulielekeza serikali kufikia elimu bora ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015 au mapema zaidi, kwa kutilia mkazo zaidi elimu ya wasichana.