Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:46 pm

NEWS: TANZANIA KUWA MWENYEJI ONESHO LA UTALII JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.


DODOMA: Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Tanzania itakuwa mwenyeji wa kwanza wa onesho la Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EARTE).



Lengo la onesho hilo hapa nchini ni kuvutia na kukuza uwekezaji katika sekta ya Utalii.




Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma , Mhe. Masanja amesema onesho hilo litakuwa linafanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kila mwaka .



"Onesho la EARTE litafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 9 hadi 16 Oktoba, 2021 ambapo litajumuisha siku tatu za maonesho na siku tano za ziara maalum ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na fursa za utalii wa ndani kwa Tanzania Bara na Zanzibar," amesema Mhe. Masanja.



Wakati huo huo ,amefafanua kuwa, kwa kutambua Utalii kama sekta mtambuka onesho hilo ni fursa muhimu ya kuhamasisha uhifadhi wa Maliasili na Malikale.