- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TALIBAN WATANGAZA SEREKALI YAO MPYA
Utawala wa Taliban umetangaza sehemu ndogo ya serikali yake mpya ambayo itaongozwa na Mohammad Hassan Akhund. Mwanzilishi mwenza wa Taliban Abdul Ghani Baradar ameteuliwa kuwa naibu kiongozi wa serikali mpya, Abdul Ghani Baradar, ambaye anaheshimiwa na kusikilizwa na makundi mbalimbali, aliongoza mazungumzo ya Doha kati ya Taliban na Marekani, ambayo yaliwezesha kuondolewa kwa vikosi vya kigeni nchini Afghanistan.
taarifa hiyo imetolewa Jumanne hii jioni na msemaji mkuu wa Taliban Zabihullah Mujahid katika mkutano na waandishi wa habari huko Kabul.
Mullah Yaqoub, mtoto wa Mullah Omar, ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi, na Sirajuddin Haqqani, mkuu wa mtandao wa Haqqani ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Sirajuddin Haqqani anaongoza tawi la kijeshi la Taliban, mtandao wa kigaidi. Mtandao wa Haqqani ndio uliohusika na mashambulio yaliyotekelezwa kwa kipini cha miaka 20 iliyopita dhidi ya vikosi vya kigeni, vikosi vya serikali ya Afghanistan na raia.
Amir Khan Muttaqi, mshauri wa Taliban huko Doha, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
"Serikali haijakamilika," alisema msemaji Zabihullah Mujahid, akihakikishia kwamba Taliban, ambayo iliahidi kuwashirikisha watu mbalimbali katikaserikalihiyo mpya, itajaribu "kuchukua watu kutoka mikoa mingine ya nchi".
Taliban imerejea madarakani miaka ishirini baada ya kuondolewa mamlakani na muungano ulioongozwa na Marekani.