November 23, 2024, 7:07 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAKUKURU INAWASHIKILIA MWENYEKITI NA KATIBU WA CCM BABATI
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Manyara inawashikilia mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Maisaka Katoi wilayani Babati Bakari Katibu na Katibu wa Tawi hilo Juma Swalehe kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya Shilingi laki mbili(200,000) kinyume cha kifungu namba 15 cha sheria ya kuzua na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kwa mujibu wa Taarifa ya TAKUKURU iliyotolewa Leo Juni 25, 2020 imesema kuwa Wawili hao waliomba Rushwa toka kwa Mwinjilisti wa Kanisa la Kilutheri la Komoto kwa maelezo kuwa baada ya kupokea fedha hizo wangemuachia kiwanja walichodai kuwa ni mali ya Chama cha Mapinduzi.