Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:49 am

NEWS: TAKUKURU IMEMKAMATA NA KUMUACHILIA ADEN RAGE

TAKUKURU mkoani Tabora imesema ilimkamata na kumuhoji aliyekuwa Mwenyekiti wa Club ya Simba na Mkurugenzi wa Voice of Tabora, Ismail Aden Rage kwa tuhuma za kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu kabla ya wakati.

Rage anadaiwa kukusanya viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wa kata na matawi kwa lengo la kuwashawishi wampigie kura katika Uchanguzi wa Mwezi Octoba mwaka huu.

Taarifa ya Takukuru iliyotolewa leo Mei 25, 2020 inasema Rage ameachiwa kwa dhamana na uchunguzi wa suala lake unaedelea na pindi utakapokamilika taarifa kamili itatolewa na Taasisi hiyo.

Takukuru Tabora imewatahadharisha wale wote wanaotaka kufanya kampeni kabla ya wakati na kutoa rushwa kuacha mara moja