- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAASISI YA BUNGE KENYA KUPITIA WAKATI MGUMU
Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa la Kenya, maspika wa mabunge yote mawili watakuwa wakishiriki kampeni za kuwania viti vingine kando na kuendesha majukumu yao.
Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi, ametangaza kuwa atawania urais huku mwenzake wa Bunge la Seneti Kenneth Lusaka akiapa kutwaa tena kiti chake cha awali cha gavana wa Bungoma.
Bw Muturi alitoa tangazo hilo Julai 4, 2021 miezi miwili baada ya kutawazwa msemaji wa jamii za eneo la Mlima Kenya; wadhifa unaoshikiliwa kwa sasa na Rais Uhuru Kenyatta.
Bw Lusaka naye ameapa kumpokonya Gavana Wycliffe Wangamati kiti cha ugavana wa Bungoma, ambacho alikishilia kati ya 2013 na 2017.
Bw Lusaka alipoteza kiti hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2017 alipokitetea kupitia tiketi ya chama tawala cha Jubilee kwa kulemewa na Bw Wangamati aliyepeperusha bendera ya Ford Kenya.
Wadadisi sasa wanahoji jinsi Muturi na Lusaka watakavyoweza kutekeleza majukumu yao ya kuongoza shughuli za bunge huku wakiendesha kampeni za kuwania nyadhifa za urais na ugavana, mtawalia.
Hii ni kwa sababu, mabunge wanayoongoza yatahitajika kushughulikia miswada na hoja nyingi zenye umuhimu kwa kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.