- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AWATAKA WABUNGE WA CCM KUITISHA KIKAO CHA KUSEMANA
Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka wabunge wote wa CCM kukutana kwenye kamati maalum ya wa Bunge wa CCM(Party Caucue) kwa lengo la kwenda kusemana na hatimaye kama kunamakundi miongoni mwao waweze kuyavunja na kurudi bungeni wakiwa wamoja.
Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao mara moja cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) na vikao vya mara kwa mara ili kama wabunge wanaamini kuwa kuna makundi ndani ya Bunge waweze kuthibitiana.
“Ili kama kweli wabunge wanaamini kuna makundi miongoni mwao mahali ambapo mnaweza kuthibitiana sio humu, kwasababu hapa ni vigumu kuyazungumza hayo. Mahali ambapo mnaweza kuzungumza na kujibiana ni kama yupo mtuhumiwa akapata nafasi ya kujibu ni kwenye cocus,” amesema.
Spika Ndugai ameongea hayo hii jana Jumatatu Aprili 19 20221 baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli
Amesema iwapo mambo ya chama wakiyahamishia bungeni wanawapa ugumu tu wa namna ya kuyaendesha.
“Maana kusema kweli kama kuna kundi na Bunge hili ni jipya sana na kundi hilo ni kundi la nini. Nahitaji kufahamu na hebu yapelekeni kule na sisi tutajifunza kwamba kuna nini. Mbona mimi naona kama kawaida tu?” amehoji.
Hata hivyo, amesema kama yanayosemwa na mbunge huyo yapo basi ni ya kina Rwekiza na msaidizi wake Naibu Katibu wa Kamati hiyo Rashid Shangazi na kuwataka kuita vikao siku za jumapili.
“Iteni kikao saa tano asubuhi watu wanapiga hadi saa 12 jioni, watu mnasemana wewee yanaisha. Sisi tulikuwa tunafanya hivyo kesho yake ikiwa Bunge tunafanya mambo ya Bunge makundi tunayaacha huko huko kwasababu katika siasa makundi si kitu cha ajabu.
Siasa ni makundi lakini mradi hayaleti sumu ambayo inatufanya tusiweze kwenda vizuri,”amesema.