- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI APIGA MARUFUKU KIGOGO KUTATWA BUNGENI
Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemzuia Mbunge wa Arusha Mjini Goodbless Lema kumtaja Mwanaharakati anayetumia Jina la kigogo kwenye mtandao wa Twitter ndani ya Bunge hilo.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo hii leo Juni 5, 2020, wakati Mbunge huyo, akichangia hoja ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo na ndipo alipotolea mfano wa baadhi ya watu kwamba wamekuwa wakikamatwa na kutakiwa kumtaja mtu anayetumia jina la Kigogo katika mtandao wa Twitter.
Mbunge Lema alisema kuwa "Sasa Mheshimiwa Spika nini kinatokea, siku hizi watu wengi wanakamatwa Kigogo ni nani Kigogo ni nani".
Ambapo Spika Ndugai alijibu, "Aaah nimepiga marufuku, huyo achana naye".
Baada ya hapo Lema aliendelea kuongea na kuwataka waliokwenye Mamlaka husika wawe wanajibu hoja zinazoulizwa katika mitandao ya kijamii.
Lema amesema kuwa ameshauri mamlaka za Serekali kuwaacha watu waendelee kukosoa mitandao.
"Msiogope matusi ya mitandaoni, tafuteni hoja za kujibu, mkiona mmepigwa mitandaoni leteni majibu, sasa mkiwazuia kabisa wataacha kukosoa mitandaoni na kuanza kukosoa kwa risasi, wacheni watu wapumue wanachosema kama siyo ukweli Waziri atoke ajibu" - amesema Gdbless Lema
Kigogo amekuwa akiikosoa vikali Serekali ya Rais Magufuli kwenye masuala mbalimbali, juu ya utendaji kazi wake na amekuwa akiwapinga na kuwazodoa wale wote wanaomuunga mkono au kumsifia Rais Magufuli.