Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:08 am

NEWS: SPIKA NDUGAI AMUOMBA RADHI RAIS SAMIA

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemuomba radhi Mkuu wa nchi wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa ujumla wake baada ya matamshi yake aliyoyatoa hivi karibuni Mjini Dodoma yaliyodai kuwa nchi itapigwa mnada kama Serekali itaendekeza kukopa kopa mikopo mbalimbali.

Amesema “Kwa hiyo binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa kwamba nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo, ninatumia fursa hii kumuomba radhi sana mheshimiwa Rais na Watanzania wote” amesema na kuongeza

“Rais ndio kiongozi wetu mkuu tutamheshimu “amesema Ndugai

Ndugai ameomba Radhi hiyo hii leo Jumatatu Januari 3, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Amesema kuwa hotuba yake haikuwa na jambo la kukashifu wala kudharau juhudi za Serikali bali alikuwa anasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.

ALICHOKESEMA NDUGAI JUU YA DENI NA NCHI KUPIGWA MNADA.

Siku ya Desemba 28, 2021 akiwa Dodoma alisema “Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai

“Tutembeze bakuli ndio heshima, tukishakopa tunapiga makofi, sisi wa kukopa kila siku, alisema Ndugai huku akiongezea kuwa "Kuna siku nchi itapigwa mnada hii,”

KAULI YA SPIKA NDUGAI HII LEO

Ndugai amesema “Katika mazungumzo yale baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya watu wakakatakata mambo, wakawasilisha ujumbe nusu, ujumbe nusu ule umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, ambao mjadala umesababisha usumbufu wa hapa na pale” amesema Ndugai nakuongeza

“Kwa hiyo niliona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa, hapakuwa na lolote la kukashifu wala kudharau juhudi zozote za Serikali, tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono”

“Katika mazungumzo yetu niliwataka wenzetu pamoja na mabo mengine tulipe kodi, ushuru na tozo mbalimbali huo ndio ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu” amesema