- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AKERWA NA KUKATIKA KATIKA KWA UMEME NA MAJI
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amesema anakerwa na tabia ya kukatika umeme na maji mara kwa mara kunakoendelea hivi sasa katika maeneo mengi nchini na kutanabaisha kuwa kitendo hicho kinatia aibu taifa kwani mataifa mengi yameshavuka hatua hiyo.
Kauli hiyo ya Spika Ndugai ameitoa Juzi wakati akichangia mada katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dodoma (RCC).
“Unakuta eti unawasha taa hakuna umeme au unafungua koki ya bomba la maji hakuna maji, hali hii haipo duniani suala kama hili la huduma wenzetu walishavuka siku nyingi mtu akifungua koki anatakiwa akute maji na siyo vinginevyo.
“Lakini hatuwezi kuwalaumu kwa sababu hatujui nini tatizo, lakini katika suala la umeme kama kule kwangu Kongwa aisee imekuwa kero kubwa sana, mara unawaka mara unakatika na tena wakisikia Simba kamfunga Yanga ndiyo haurudi kabisa,” alisema kwa utani.
Kadhalika, Ndugai aliwataka wajumbe wa kikao hicho kuweka mikakati ya kwenda kukabiliana na kero ya mimba za utotoni.
Alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika kikao hicho, mimba za utotoni zimeongezeka kila mwaka hali ambayo inahitaji juhudi kuchukuliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel, alisema Shirika la Umeme nchini linatakiwa kubadilika kwa kuwa hali hiyo inachonganisha wananchi na serikali yao.
Alisema Wilaya ya Kongwa hivi sasa upo uwekezaji wa viwanda, lakini kutokana na hali ya kukatika kwa umeme inaathiri shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.