- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI ACHUKIZWA KITENDO CHA POLISI KUWEKA WATU NDANI
Dodoma. SPIKA wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, ameonyesha kuchukizwa na Tabia ya baadhi ya Polisi kukamata watu hovyo hovyo hata wengine ambao wana heshima zao na wanajulikana mahali wanapoishi lakini wanarundikwa tu rumande pasipokuwa na ulazima wowote.
"Inatakiwa tujifunze kwa nchi za wengine ambapo mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka watu ndani ni raha"
"Hiki kitu binafsi kinaniuma sana, mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote" amesema Ndugai.