- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA ATOA TENA UFAFANUZI WA NAMNA YA KUFUKUZA WABUNGE
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Ijumaa Mei 7, 2021 amesisitiza kuhusu wabunge 19 waliofukuzwa uanachama Chadema, akitaka kupatiwa vielelezo kuhusu kufukuzwa kwao na kwamba huo ni msimamo wa kiti.
Katika maelezo yake Spika Ndugai amesema kuwa kwa chama chochote cha siasa chenye lengo la kuwafuvua ubunge wanachama wake, lazima kifuate taratibu zifuatazo, kwanza Katibu wa chama husika lazima amuandikie Barua spika ikiambatana na Muhtasari wa kikao chenye wajumbe halali na Nakala ya katiba ya Chama husika.
Ndugai amesema: "Hata akija Spika mwingine bado msimamo utakuwa ni huohuo, lazima kuwepo na viambatanisho ili na mimi niwasiliane na msajili wa vyama vya siasa tujue kama kamati iliyotoa uamuzi ina haki au vinginevyo,".
Aidha, Ndugai amesisitiza kuwa angalizo hilo haliwalengi wabunge wa upande mmoja tu bali kwa chama chochote cha siasa ambacho kitakuwa na nia ya kuwatimua wabunge
Chama cha Chadema, Ijumaa ya Novemba 27, 2020 kiliwavua uanachama wanachama wake 19 akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza la wanawake Bawacha Halima Mdee walioapishwa kuwa Wabunge wa viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Uamuzi huo ulitokana na maazimio ya Kamati Kuu iliyokutana Novemba 27 Jijini Dar es Salaam.
Wengine walifuluzwa Chadema ni Esther Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera alisema katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika alimuandikia barua Novemba 19, 2020 yenye orodha ya majina ya wanachama wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum na kwamba tume hiyo ilitumia orodha hiyo kuteua wabunge wa viti hivyo