- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA AKERWA NA WATU KUJIITA Dr. INJINIA, WAKILI MSOMI
Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amesema anakerwa sana na baadhi ya watu kujikweza na fani zao walizosomea kama wahasibu, wahandisi, mawakili na madaktari wa kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo chake wakati si lazima iwe hivyo. Na kuona wenzao kama hawajasoma.
Spika amezotelea mfano kama, mawakili hujiita wakili msomi, wahasibu hupenda kuanza na neno CPA, wahandisi hutumia neno la ‘Engineer’ na waliosoma shahada za uzamivu (PhD) majina yao huanza na neno Dk
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Septemba 1, 2021 bungeni katika kipindi cha mjadala wa hoja za wabunge kuhusu muswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi.
Amesema anajua atashambuliwa na mawakili mitandaoni lakini anataka kujua iwapo hawaoni aibu kujiita ni wasomi wakati nchi ina wasomi wengine.
“Najua watanishambulia katika mitandao, ..ah lakini huo ndiyo ukweli nani asiyekuwa msomi katika nchi hii, au wengine hawajasoma, kwani hamuoni aibu fulani hivi kujiita wasomi wakati kuna wengine katika nchi hii wamesoma,” amehoji Ndugai.
Spika amesema; “kuna wakati nitahitaji mnishauri kuhusu hili la wanasheria kujiita wakili msomi, huu ni utaratibu fulani ulioanzishwa na wenzetu Waingereza wa kutukuza baadhi ya kada,’’
Kuhusu mawakili amehoji kama wakibaki na neno la wakili watapungukiwa kitu gani huku akiweka wazi kuwa neno msomi linawaongezea kitu gani kwa Watanzania wasiopenda kujikweza katika mambo mengine.