- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SITA MBARONI KWA KUTAKATISHA FEDHA ZA BENKI YA NBC
Dar es Salaam. Watu sita wakazi wa Dar es salaam wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya kughushi, kuongoza genge la uhalifu, kutakatisha fedha na kujipatia kwa njia ya udanganyifu Sh4.7 bilioni mali ya benki ya NBC.
Walioshtakiwa ni meneja uzalishaji wa kampuni ya Peertech Limited, Leena Joseph (39); mfanyabiashara Bernard Mndolwa (47) na ofisa wa benki, Salvina Karugaba (46).
Wengine ni Baraka Madafu (39), Mark Mposo (40), Lusekelo Mbele(39).
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo Februari 25, 2021 na jopo la mawakili wawili likiongozwa na wakili mkuu wa Serikali, Paul Kadushi akisaidiana na Wankyo Simon mbele ya hakimu mkazi mkuu, Kassian Matembele.
Akiwasomea mashtaka yao, wakili Simon amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 13/2021.
Wakili Simon amedai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Desemba 4, 2018 na Desemba 31, 2020 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Katika shtaka la kwanza wakili Simon amedai kati ya Desemba 4, 2018 na Desemba 31, 2020 washtakiwa hao walitenda kosa la kuongoza genge la uhalifu na kwa udanganyifu wakajipatia Sh4.7 bilioni.
Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, washtakiwa wanaodaiwa siku na maeneo hayo walijipatia Sh4.7 bilioni kutoka Benki ya NBC baada ya kuwasilisha nyaraka za uongo wakionyesha kuwa watu 78 ni wananufaika wa kampuni ya Peertech Company Limited wakati wakijua kuwa ni uongo.
Baada ya kusomewa mashtaka yao Wakili Kadushi amedai upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Matembele ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 12, 2021 huku washtakiwa wakirudishwa rumande
kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.