Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:23 am

NEWS: SIMBACHAWENE AAGIZA POLISI KUMUHOJI ASKOFU MWINGIRA

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene amemuamuru kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kumtafuta Askofu wa Kanisa la Efatha Josephat Mwingira ili kumhoji juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa kwenye ibada ya Chrismas.

Simbachawene ametoa kauli hiyo hii leo Jumatatu Desemba 27, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali ya nchi.

“Kumetokea tamko la kiongozi mmoja Askofu Mwingira na mimi nimelisikia kwenye mitandao lakini pia nimepata ile clip lakini sijasikia vizuri maana kama haina sauti bado tunaendelea kulifuatilia"

“Ni tuhuma nzito sana na zinapotolewa na kiongozi ambaye ni wa kijamii,dini,maarufu na anajulikana tunapata shida kidogo kwasababu kama matukio yote kama alivyosema ndivyo ilikuwa inatokea ni kwanini basi alikuwa hatoi taarifa polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa,” amesema Waziri Simbachawene.

Aidha Simbachawene amesema kuwa “Nchi yetu ni nchi inayoongozwa kwa utawala wa haki na sheria,mtu hawezi kukaa akiwa na hofu na maisha yake na pengine akaenda katika hatua kama alivyozisema Askofu Mwingira halafu likaachwa hivi hivi ninadhani ipo haja tupate zaidi na zaidi,”

“kama aliyoyasema(Mwingira)ni kweli tutahitaji atusaidie kutupa taarifa zaidi,si vibaya pia RPC DSM kumtafuta ili kupata maelezo zaidi,tumesikia anazungumza na waumini wake lakini tungetamani tusikie anaingia kwenye rekodi ili pale inapowezekana tuweze kushughulikia” amesema Waziri Simbachawene