Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 4:41 pm

NEWS: SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA MPYA.

Club ya Simba SC imemtangaza Muhispaniola Pablo Franco mwenye umri wa miaka 41 kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.

Pablo Franco amesaini kandarasi ya miaka 2 kuitumikia club hiyo.

Pablo anachukua nafasi ya Didier Gomez ambaye mkataba wake ulisitishwa wiki mbili zilizopita.

Pablo alikuwa anafundisha club Al Qadsia ya Kuwait kabla ya kuja kwa wana kariakoo Simba Sport Club.

Kocha huyo raia wa kihispania amewahi kuifundisha club ya ligi kuu ya Hispania ( La Liga) ya Getafe.

Aidha Pablo amewahi kuwa kocha msaidizi kwenye club kubwa kabisa inaongoza kwa mataji mengi ya ligi ya Mabingwa ya ulaya (UEFA Champions League) Real Madrid.