- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ?SIMBA WATAMBULISHA JEZI MPYA
Dar es salaam. Klabu ya Soka ya Simba leo hii Sept 3, 2021 imezitambulisha Jezi zake sambamba na kuanza kuuza jezi hizo zitakazotumiwa na klabu hiyo kwa msimu wa mwaka 2021/2022.
Kuanza kuuzwa kwa Jezi hizo kunakuja siku moja kabla ya uzinduzi rasmi wa jezi hizo kutokana na mahitaji ya mashabiki wa klabu hiyo.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga amewaambia waandishi wa habari leo kuwa jezi hizo zinapatikana nchi nzima.
Aidha, Kamwaga amesema kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayosindikiza Wiki ya Simba ambayo inatarajiwa kuadhimishwa kuanzia Septemba 13 mpaka Septemba 19 kwenye hafla ya kilele cha siku ya Simba.
Kuhusu kuvuja kwa Jezi ya Klabu hiyo, Kamwaga amesema sio jambo la ajabu na hata vilabu vikubwa barani Ulaya vimekuwa vikikabiliwa na tatizo hilo.
JEZI ZINGINE NI HIZI, ambapo kuna Away Kit na Home kiti.