- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHULE YA KIMATAIFA MOSHI YAFUNGWA KWA CORONA
Shule ya kimataifa ya UWCEA kampasi ya Moshi, Tanzania imelazimika kusitisha mafunzo yake ya ana kwa ana baada ya mwanafunzi mmoja wa shule hiyo kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Shule hiyo ya kimataifa iliyopo kaskazini mwa Tanzania sasa itaanza kufanya mafunzo yake kwa njia ya kidijitali hadi Februari mosi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shule hiyo Januari 18 mwanafunzi huyo alithibitishwa kuwa na corona na jana Jumanne mwanafunzi mwingine ameonesha dalili za maambukizi ya virusi hivyo, lakini bado haijathibitishwa kitabibu kama ana maambukizi ya ugonjwa huo.
Kumekuwa na taarifa za sintofahaumu kwenye mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa ugonjwa huo nchini Tanzania licha ya Serekali ya nchi hiyo kutangaza kuwa hakuna Corona.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza kila anapopata nafasi kwa umma kuwa Nchi yake haina ugonjwa wa Corona, na kuwataka Raia wake kufanya kazi.
Akiwa mkoani Kagera jana Jumanne rais John Magufuli amesihi wakulima nchini humo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula akibashiri uhaba wa chakula duniani baadaye mwaka huu kwasababu ya janga la virusi vya corona.
"Mwaka huu kuna uwezekano wa kutokea kwa baa kubwa la njaa duniani kwa sababu watu wengi wanazingatia hatua za kutotoka nje kujikinga dhidi ya corona, lakini hilo halistahili kutukatisha tamaa kwasababu hata sheria hizo zikiwekwa bado watahitaji kula, tutakuza mazao na kuyauza."
Takwimu rasmi ya idadi ya maambukizi na vifo vya corona ilitolewa kwa mara ya mwisho mwezi Aprili 2020, kufikia mwezi Juni rais Magufuli akatangaza kuwa "corona imekwisha Tanzania kutokana na maombi ya wananchi."
Tanzania imekosolewa vikali kutoka pande mbalimbali ikiwemo na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa namna ilivyokabiliana na janga hilo.